21 Mei 2015 - 18:49
Jeshi la Burundi latoa wito wa umoja

Waziri wa ulinzi wa Burundi amelitaka jeshi leo kuonesha mshikamano baada ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi wakati majeshi ya usalama yakipambana kuzuia wiki kadhaa za maandamano ya ghasia ya kuipinga serikali.

Mtu  mmoja  ameuwawa  leo katika  mapambano  na  polisi  katika mji  mkuu  Bujumbura, ameeleza  mtu  aliyeshuhudia , akiwa  mhanga wa  hivi  karibuni  kabisa  wa  ghasia  zilizozuka  kutokana  na  juhudi za  rais Pierre Nkurunziza  kuwania  muhula  wa  tatu  madarakani, ambapo  zaidi  ya  watu  20  wamefariki.

Waziri  wa  ulinzi aliyeteuliwa  hivi  karibuni  Emmanuel Ntahonvukiye ametoa  wito  wa  umoja  baada  ya  jaribio  hilo  la  mapinduzi, ambalo  lilizimwa  na  majeshi  tiifu baada  ya  mapigano  mitaani  kati ya  makundi  hasimu ndani  ya  jeshi  hilo.

Hali bora ya  Burundi  kama  taifa  inategemea  maelewano  ya jeshi,  taarifa ya  jeshi  imesema,  na  kuonya  kwamba  iwapo  jeshi litatengana , hali  hiyo  itasababisha  hali  kama  inayoonekana katika  nchi  iliyoharibiwa  kwa  vita  ya Somalia.